Waziri Mkuu
Mhe. Kassim Majaliwa amesema katika kufanya jitihada za uokoaji, ameagiza mitungi
ya gesi ya oksijeni kutumika kwa ajili ya kupeleja hewa safi kwa waliokwama kwenye
vifusi.
Waziri Mkuu
ametoa kauli hiyo leo Novemba 16, wakati alipofika Mtaa wa Kongo, Kariakoo
kufuatia tukio la jengo la ghorofa kuporomoka na kufukia baadhi ya
wafanyabiashara na wateja.
"Uzuri
tunaambiwa kuwa baadhi ya familia zinapata mawasiliano na ndugu walioko huko
chini (kwenye vifusi). Kwa hiyo jitihada zinaendelea za kuwaokoa waliopo huko
chini, tuhakikishe hatutumii nguvu bali tunatumia akili zaidi ili tuweze kuokoa
maisha yao.”
"Kwa
sasa wanakosa hewa lakini tumeandaa utaratibu wa kupeleka oksijeni kiasi cha
kutosha ili waliopo kule waweze kudumu kwa muda mrefu, wakati tukiendelea na
zoezi la uokoaji," amesema Mhe. Majaliwa.
Ameeleza
kwamba katika zoezi hilo la uokoaji hadi anapoongea jumla ya watu 28 walikuwa
wameshaokolewa wakiwa hai na kupelekwa hospitali kupatiwa matibabu, huku mtu
mmoja akithibitishwa kufa.
0 Maoni