Hospitali
Kuu ya Taifa ya Muhimbili imethibitisha kupokea majeruhi 40 wa ajali ya
kuporomoka kwa ghorofa iliyotokea mapema leo Kariakoo Mtaa wa Kongo jijini Dar
es Salaam.
Mkurugenzi
Mkuu wa hospitali hiyo Prof. Mohamed Janabi amesema tayari majeruhi 32 kati ya
hao wamepatiwa matibabu na kuruhusiwa kurejea nyumbani huku wengine wanane
wakiendelea kupatiwa matibabu.
Pamoja na Muhimbili,
hospitali nyingine za umma zinazozendelea kupokea majeruhi wa ajali hiyo na
kuwahudumia ni hospitali ya rufaa ya wilaya ya Ilala, Amana pamoja na hospitali
ya Mnazi Mmoja.
0 Maoni