Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Hazara Chana (Mb) ameweka jiwe la
misingi la ujenzi wa mradi wa miundombinu ya Ngorongoro Lengai Geopark
wenye thamani ya shilingi bilioni 25 unqofadhikiwa Serikali ya jamhuri ya China kwa lengo la kuongeza zao la utalii wa
Jiolojia nchini (Ngorongoro Lengai UNESCO Geopark).
Hafla hiyo
imefanyika Karatu, Mkoani Arusha, leo Novemba 16, 2024 ambapo Mhe. Chana amesema ujenzi wa makumbusho hiyo
ushuhuda wa maono ya Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ukuaji wa sekta ya
utalii na uhifadhi wa mazingira hapa nchini.
Balozi
wa China nchini Tanzania, Mhe. Chen Mingjian amesema utekelezaji wa
mradi huo unatokana na uhusiano mzuri wa kidiplomasia kati ya Tanzania na China
na ndio unaoleta matokeo ya kuboresha miundombinu ikiwemo sekta ya utalii.
‘‘Ushirikiano
kati ya Tanzania na China umeimarika vya kutosha na niwahakikishie kuwa
Serikali ya China itaendelea kushirikiana na Tanzania kusaidia ujenzi wa miradi
mbalimbali hususan katika maendeleo ya sekta ya utalii," amesema Mhe.
Chen.
Kamishna wa
Uhifadhi NCAA Dkt. Elirehema Doriye amesema kuwa Mradi wa makumbusho hiyo wenye
hadhi ya viwango vya dunia utakapokamilika, utasaidia watalii kutoka mataifa
mbalimbali kufurahia zao la utalii wa miamba kutokana na vivutio vitakavyokuwa
katika makumbusho hiyo ambapo wakazi wa wilaya za Karatu, Ngorongoro, Monduli
na Longido watakuwa sehemu ya wanufaika wa mradi huo.
Akitoa
taarifa ya Utekelezaji wa mradi huo, Afisa Uhifadhi Mkuu anayesimamia idara ya
urithi wa Utamaduni na Jiolojia PCO Dkt. Agness Gidna ameeleza kuwa makumbusho
hiyo itakapokamilika itakuwa maelezo ya vituvio mbalimbali ikiwemo Urithi wa
Jiolojia unaopatikana katika eneo la Ngorongoro, taarifa zilizohusu milima na
mabonde/Kreta za Ngorongoro zilivyotokea, wanyama waliopo, mioto ya asili, Mito
na maji na umuhimu wake kwa jamii zinazozunguka Ngorongoro.
Vituvutio
vingine vitakavyokuwepo katika makumbusho ni Urithi wa Malikale unapatikana
Ngorongoro, Utamaduni wa jamii za Wawindaji, na ukumbi wa maonesho unaobeba zaidi
ya watu 100 kwa ajili kuona Ngorongoro live.
Mwenyekiti
wa Bodi ya NCAA Jenerali Venance Mabeyo (Mst) ameainisha kuwa bodi ya NCAA
pamoja na Menejimenti zinashirikiana na Mkandarasi wa makumbusho hiyo
kuhakikisha kazi inafanyika kwa viwango vya Kimataifa, kuzingatia ubora na
kuhakikisha kufikia mwezi Mei, 2025 jengo hilo liwe limekamilika na watalii
kuanza kupata huduma kupitia vivutio vitakavyokuwepo katika Makumbusho hiyo.
Katibu Mtendaji wa UNESCO Tanzania Prof. Hamis Malebo amebainisha kuwa hifadhi ya Miamba ya Ngorongoro ndio hifadhi kubwa na yenye maajabu makubwa Barani Afrikka kutokana na uwepo wa Kreta mbili za ajabu na volcano hai, ambapo Nchi ya Tanzania ni ya pili barani afrika kuwa na hadhi ya Jiopaki inayotqmbuliwa na UNESCO ikitanguliwa na Morocco.
Na. Kassim Nyaki- Karatu
0 Maoni