Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu ametoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki, wasanii na wapenzi wote wa muziki nchini kufuatia kifo cha Mwanamuziki nguli Boniface Kikumbi Mwanza Mpango ‘King Kikii’ ambaye amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Novemba 15,2024 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Rais Samia
amesema “Kwa zaidi ya miaka 50 King Kikii ametoa burudani kwa mamilioni ya
Watanzania, na amekuwa Mlezi na Mwalimu wa wengi katika tasnia ya muziki,
tutamkumbuka na kumuenzi kwa kazi zake nyingi na nzuri ikiwemo wimbo wake
maarufu wa ‘Kitambaa Cheupe’ ambao umeendelea kuwa sehemu ya burudani kwenye
maeneo na shughuli mbalimbali za burudani nchini.”
“Mwenyezi
Mungu ailaze roho yake mahali pema, Amina”
0 Maoni