Naibu Waziri
Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko leo Novemba 17, 2024 amefanya
ziara Wilayani Mtwara na kukagua ujenzi wa miradi inayotekelezwa kwa fedha
zinazotolewa na wawekezaji mbalimbali kwa ajili ya kuboresha maendeleo kama
njia ya kurejesha rasilimali kwa wananchi kupitia (CSR).
Akikagua
Kiktuo cha Afya Msimbati, Dkt. Biteko ameeleza kutoridhishwa na matumizi ya
fedha iliyokuwa imepangwa kutumika katika ujenzi wa kituo hicho na kupelekea
ongezeko la kiasi cha shilingi milioni 159.
Kituo hicho
cha Afya awali kilikadiriwa kujengwa kwa gharama ya shilingi milioni 600 lakini
gharama za ujenzi huo ziliongezeka hadi kufikia shilingi milioni 759 na hivyo
kuibua maswali ambayo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Mtwara, Abeid Kafunda
amekiri kuwa hajui sababu za ongezeko la gharama hizo.
Aidha, Dkt.
Biteko ameiagiza Taasisi ya Kuthibitj na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani
Mtwara kufanya uchunguzi wa kina kuhusu sakata la Kituo cha Afya cha Msimbati
baada ya kubaini kuwa ujenzi wa mradi huo hauendani na thamani halisi ya fedha
pamoja na kuchukuliwa hatua kali kwa wahusika wote wa usimamizi Mradi na
kusababisha ongezeko kubwa la fedha tofauti na maeneo mengine nchini ambayo
vituo vya Afya vinajengwa kwa thamani ya shilingi milioni 500 hadi 600.
Baadae, Dkt.
Biteko alifanya ukaguzi wa majengo ya Kituo cha Afya Msimbati ambacho ujenzi
wake umekamilika kwa asilimia 98 na kuwataka watekelezaji wa miradi mbalimbali
nchini kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa kuzingatia kwamba miradi hiyo
inakusudiwa kuwanufaisha Watanzania na sio vinginevyo, amesema Dkt. Biteko
Akizungumzia
hali hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Kanali Patrick Sawala amesema uongozi
wa Mkoa umekuwa ukifanya ziara ya kukagua miradi hiyo inayojengwa kutokana na
utekelezaji maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.
Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara
inakotoka gesi wananufaika na rasilimali hizo kupitia CSR.
Katika hatua
nyingine, Mheshimiwa Dkt. Biteko amekagua ujenzi wa Kituo cha Polisi Kata ya
Msimbati ambacho kimekamilika na maombi ikiwa ni ujenzi wa Uzio, samani, mifumo
wa ya TEHAMA na, maji nyumba ya makazi ya Mkuu wa Kituo.
Wakazi wa
Mikoa ya Lindi na Mtwara wamekuwa na kilio cha muda mrefu wakiomba huduma za
maendeleo kutokana rasilimali ya gesi kuchimbwa katika mikoa hiyo suala
lililoisukuma Serikali kuagiza TPDC kutoa fedha kupitia CSR ili iweze
kunufaisha wananchi kama inavyotokea katika maeneo mengine ya nchi.
Kufuatia maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko alielekeza kujengwa kwa kituo cha Afya katika eneo la Msimbati, Kituo cha Polisi pamoja na Uwekaji wa taa za Barabarani katika eneo hilo.
Na. Ofisi ya
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati
0 Maoni