Mtendaji
Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mhandisi Victor
Seff amewaagiza Mameneja wa TARURA wa Wilaya kote nchini kukagua na
kusafisha madaraja na makalavati yote
katika maeneo yao ili yaweze kupitisha maji kwa urahisi na kuepusha
mafuriko.
Mhandisi Seff
ametoa maagizo hayo wakati wa ziara yake katika wilaya za Nachingwea, Liwale na
Ruangwa na kusema kwamba msimu wa mvua umeshaanza katika maeneo mengi hapa nchi
hivyo kwa kufanya usafi huo itasaidia kulinda miundombinu hiyo iliyotumia fedha
nyingi za walipa kodi.
“Kila Meneja
anapaswa kukagua na kufanya usafi kwenye madaraja na makalavati katika maeneo
yake ili mvua zinaponyesha isikwamishe shughuli za kiuchumi na kijamii kwa
wananchi endapo madaraja au makalavati yatasombwa na maji,”alisisitiza Mhandisi
Seff.
Aliongeza
kusema kwamba kutokufanya hivyo ni uzembe ambapo itai itaisababishia Serikali hasara kwa
kutenga tena fedha za ujenzi.
Aidha,
amesema hatosita kuchukua hatua kali kwa Mameneja hao kwa uzembe utakaopelekea madaraja kusombwa na mafuriko.
Agizo hilo
amelitoa Mhandisi Seff hivi karibuni wakati alipotembelea Wilaya za Nachingwea,
Liwale na Ruangwa Mkoa wa Lindi.
Naye, Meneja
wa TARURA Mkoa wa Lindi Mhandisi Fanuel Kalugendo aliahidi kusimamia na
kufuatilia agizo la Mtendaji Mkuu na kutoa taarifa baada ya kazi kukamilika.
Mhandisi
Seff yupo ziara ya kikazi ya kufuatilia miradi ya ujenzi na matengenezo ya
miundombinu ya barabara mkoani Lindi.
0 Maoni