Kamati ya
Pamoja ya Wataalamu ya Uimarishaji Mpaka wa Tanzania na Burundi (JTC)
imetembelea Mto Malagarasi ambao ni sehemu ya mpaka wa kimataifa kati ya nchi
hizo mbili ili kujionea hali halisi ya eneo hilo.
Uamuzi wa
kutembelea eneo hilo la mto Malagarasi ni sehemu ya programu ya kikao cha JTC
kinachoendelea katika halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma.
Kikao hicho
pamoja na mambo mengine kimepanga kutembelea katika vijiji vya Bukililo na
Nyakayenzi upande wa Tanzania na kijiji cha Kamusha nchini Burundi.
Timu hiyo ya
wataalamu ambayo kwa upande wa Tanzania iliongozwa na Mkurugenzi Msaidizi idara
ya Upimaji na Ramani Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Samwel
Katambi huku upande wa Burundi ikioongozwa na Meja Jenerali Mbonimpa Maurice.
Lengo la
kutembelea mpaka huo wa kimataifa ni kuwezesha JTC Kuandaa bajeti na mpango
kazi wa uimarishaji mpaka wa kimataifa baina ya nchi hizo mbili.
Kikao cha
Pamoja cha Wataalamu (JTC) kimeanza siku ya jumatatu tarehe 18 Novemba 2024 na
kimemalizika Ijumaa tarehe 22 Novemba 2024.
Zoezi la
uimarishaji mipaka ya kimataifa ni utekelezaji wa makubaliano ya umoja wa
Afrika kuwa ifikapo mwaka 2027 mipaka baina ya nchi za afrika iwe imeimarishwa.
Kiongozi wa
wa timu ya Tanzania Bw. Samwel Katambi (wa pili kushoto) akifafanua jambo
wakati wa Kamati ya Pamoja ya Wataalamu wa Uimarishaji mpaka wa Tanzania na
Burundi (JTC) ilipotembelea eneo la Mto Malagarasi uliopo wilayani Kasulu mkoa
wa Kigoma. kushoto ni kiongozi wa timu ya wataalamu kutoka Burundi Mhe. Meja
Jenerali Mbonimpa Maurice.
0 Maoni