Mjumbe wa
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, ambaye pia ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri
wa Nishati, Mhe.Dkt. Doto Biteko amewataka wananchi wasisahau safari
iliyowafikisha katika nchi ya amani na maendeleo.
Dkt. Biteko
amesema hayo Novemba 22, 2024 katika wakati akizungumza kwenye mkutano wa
Kampeni za Serikali za Mitaa zilizofanyika katika Kata ya Lulembela, Wilaya ya
Mbogwe, Geita.
Amewataka
kujitokeza kuwachagua viongozi wenye maono na mwelekeo wa kuwaunganisha kuanzia
ngazi ya shina hadi Taifa. “Tunachagua viongozi wenye uelewa wa matatizo na
kujua namna ya kutatua matatizo ya wananchi,” amesema Dkt. Biteko.
Wanambogwe
mna haki ya kuchagua Chama chenye Sera
zinazotekelezeka ambacho ni Chama Cha Mapinduzi na kuachana na wale wenye
porojo na maneno maneno, kwa kuwa watu
wangependa kupata maendeleo na wamechoshwa na maneno yanayolenga kuwagawa watu.
“Wenzetu wanakuja kusema na kutukana watu” watu wa Mbogwe ikifika tarehe 27
jitokezeni kwenda kupiga kura” Hatuhitaji ushindi wa kubebwa, bali watu
waliojiandikisha wajitokeze kupiga kura.
“Nimekuja
kuwaomba mtuunge mkono kwa kupiga kura na kuchukua vijiji na vitongoji vyote,”
ameomba.
Naye
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita, Nicolaus Kasendamila amewashukuru wagombea
waliopitishwa na kusema hadi sasa CCM imesimamisha wagombea bila kupingwa kwa
asilimia 84 katika ngazi mbalimbali katika uchaguzi huu.
Katibu wa
CCM Wilaya ya Mbogwe amesema wagombea 301 kati ya 335 CCM hawakupata upinzani
na wagombea 70 kati ya 87 katika ngazi ya vijiji wamepita bila kupingwa.
Mbunge wa
Mbogwe, Mhe. Nicodemas Maganga amewapongeza wanaCCM walioteuliwa kugombea
katika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama hicho.
Amewaomba
kuondokana na vitendo vyote vya uvunjifu wa maadili ikiwemo vitendo vya rushwa.
Amesema
wilaya hiyo inapendeza kwa vile kuna karibu kila kitu, kama kuna mapungufu ni
madogo. “ Wagombea mmeaminiwa na watu hivyo mtatakiwa kufanya kazi bila
kumruhusu shetani,” amesema.
Hata hivyo,
amewataka kushirikiana na kutowabagua wapinzani katika kuleta maendeleo ya watu
ambao ndio lengo la CCM.
“Mgeni rasmi
umechangia kuleta maendeleo ya Wilaya ya Mbogwe nasi tunakuomba ukamwambie
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kuwa
tuko imara kutafuta maendeleo ya wananchi na tunamuunga mkono,” amesisitiza.
0 Maoni