Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Oktoba 26, 2024 amekabidhi magari mapya 10 ikiwa ni ishara ya kukabidhi magari 88 yaliyonunuliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) ambayo yatasambazwa mikoani kwa lengo la kuongeza tija na kuboresha utendaji kazi wa Taasisi hiyo.
Akitoa taarifa ya magari hayo,
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Crispin Chalamila amemweleza Waziri Mkuu kuwa
katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan
madarakani, TAKUKURU imepatiwa jumla ya Shilingi bilioni 30 za kununulia magari
195 ambapo 88 ameshanunuliwa.
“Mchakatio wa kununua magari 107
yaliyobakia unaendelea na tunatarajia kuyapata hivi karibuni, tunaahidi
kutatunza magari haya ili kuongeza tija katika utendaji wetu,” amesema Bw.
Crispin.



0 Maoni