Mtangzaji wa Wasafi FM Dida kuzikwa leo Dar

 

Mwili wa aliyekuwa mtangazaji wa kituo cha redio cha Wasafi FM, Khadija Shaibu maarufu kwa jina la ‘Dida’ unatarajiwa kuzikwa leo Oktoba 5, 2024 kwenye makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa, mwili wa marehemu Dida utaswaliwa katika Msikiti wa Maamur, Upanga baada ya Salat Dhuhr ‘Saa saba mchana’ nakuzikwa saa 10 Alasiri.

Dida aaifariki dunia jana Oktoba 4, 2024 katika Hospitali ya Taifa (Muhimbili) alipokuwa akipatiwa matibabu.



Chapisha Maoni

0 Maoni