Mtangazaji wa Wasafi FM Dida afariki dunia

 

Aliyekuwa Mtangazaji wa Kipindi cha Mashamsham cha Wasafi FM, Khadija 'Dida' Shaibu, amefariki dunia usiku wa leo Oktoba 4, 2024 wakati akipata matibabu katika Hospitali ya Muhimbili.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na mtangazaji mwenzake, Maulid Kitenge, kupitia mtandao wa X, Dida alikuwa amelazwa Hospitalini hapo baada ya kuugua.



Chapisha Maoni

0 Maoni