Kampeni ya miaka minne ya Dk. Mwinyi yazinduliwa

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikulu, Mhe. Ali Suleiman Ameir Mrembo amesema Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi, atazindua miradi ya maendeleo na kuzungumza na wananchi katika mikutano na makongamano mbalimbali.

Waziri Mrembo ameyasema hayo leo, tarehe 18 Oktoba 2024, katika viwanja vya Ikulu Zanzibar, alipozindua rasmi kampeni ya Miaka Minne ya Rais Dk. Mwinyi pamoja na nembo maalum.

Aidha, Waziri Mrembo ameeleza kuwa kampeni hiyo itaanza rasmi kuanzia tarehe 21 Oktoba 2024 hadi tarehe 16 Novemba 2024.

Halikadhalika, Waziri Mrembo amesema kampeni hiyo itawafikia wananchi kupitia teknolojia ya habari, ikiwemo televisheni, mitandao ya kijamii, magazeti, na redio za kijamii.

Naye Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC), Ramadhan Bukini, amesema kampeni hiyo itajumuisha Mawaziri na Watendaji mbalimbali wa Serikali, ambao watazungumzia mafanikio ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika kila sekta, kupitia mahojiano yatakayofanyika katika Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC).



Chapisha Maoni

0 Maoni