Feri yazama ikiwa na abiria 278 na kusababisha vifo 78

 

Watu wapatao 78 wamekufa maji baada ya Feri kuzama mita chache kabla ya kufika safari yake katika Ziwa Kivu, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Feri hiyo ilikuwa ikisafiri kutokea mji wa Minova Kusini mwa Kivu na kuzama wakati ikiwasili katika fukwe ya Goma siku ya Alhamis asubuhi.

Picha ya video iliyosambazwa ilionyesha Feri hiyo ikiegemea upande mmoja na kisha kuzama majini.

Wakati Feri hiyo ikizama ilikuwa na abiria 278 kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mamlaka inayosimamia usafiri wa majini.

Matukio ya ajali za majini ni ya kawaida katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambapo Feri hujaza watu wengi kupita uwezo wake na huwa hawapatiwi jaketi za kujiokolea.

Chapisha Maoni

0 Maoni