Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mashoeshoe Mjini Maseru nchini Lesotho leo tarehe 04 Oktoba 2024.
Dkt. Mpango anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika sherehe za Miaka 58 ya Uhuru wa Lesotho na Miaka 200 ya kuanzishwa kwa Ufalme wa Lesotho zitakazofanyika katika Uwanja wa Setsoto Mjini Maseru.
0 Maoni