Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi
wa Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda kwa niaba ya Mhe Rais na Amiri Jeshi
Mkuu Dkt Samia Suluhu Hassan amewavisha nishani mbalimbali Majenerali, Maafisa
na Askari wa Pemba na Unguja Zanzibar tarehe 25 Oktoba 2024.
Nishani hizo ni Nishani ya Utumishi
Uliotukuka, Nishani ya Utumishi Mrefu, Nishani ya Utumishi Mrefu na Tabia
Njema, Nishani ya Miaka 60 ya Muungano pamoja na Nishani ya Miaka 60 ya JWTZ.
Aidha, Jenerali Mkunda amewavisha
nishani ya Jumuiya ya SADC Maafisa na Askari walioshiriki Ulinzi wa Amani
nchini Msumbiji chini ya mwavuli wa Jumuiya hiyo.
0 Maoni