Waziri wa
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy
Gwajima ametunukiwa Tuzo maalum na Taasisi ya Jamii Forums kama kiongozi
anayepokea maoni ya wananchi na kuyafanyia kazi kupitia majukwaa ya kidijitali.
Tuzo hiyo
imetolewa na Taasisi hiyo jana Septemba 21 jijini Dar Es Salaam katika tukio la
kuwatunikiwa wadau wa Jamii Forums walioandika 'Stories of Change' zitakazoleta
mabadiliko katika jamii .
Aidha Waziri
Dkt. Gwajima amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia
Suluhu Hassan aliyemuamini na kumpa nafasi na fursa ya kutumikia jamii kupitia
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum.
Vilevile,
Waziri Dkt. Gwajima amesema Tuzo hiyo imechangiwa watumishi wake wote wa Wizara
ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum na na wale wa Wizara za kisekta ambao hupokea na
kuyafanyia kazi maelekezo yake kufuatia maoni na hoja za wananchi ambazo
amekuwa akizipokea kutoka kwenye Jukwaa la Jamii Forums.
"Heshima
hii iende kwa familia yangu na mume wangu mpenzi Advocate Gwajima ambaye, amekuwa akinipa ushirikiano mkubwa
wakati wote wa kutumia hata muda wa familia kwa ajili ya kufuatilia hoja za
wananchi kwenye Jukwaa hili," amesema Waziri Dkt. Gwajima.
Pia ameahidi
kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na Wananchi kwa nafasi yake,
na kuhakikisha sauti zote za wananchi zinasikilizwa na kufanyiwa kazi kadri
inavyowezekana.
Amesisitiza
kila mmoja ana nafasi muhimu katika mchakato wa uamuzi, na ni wajibu wa kila
mmoja kama viongozi kusikiliza na kujibu yote yale yanayohitaji majibu kwa
wananchi kwani tunapofanya kazi pamoja, tunafanikisha kuchochea maendeleo na
kuboresha maisha ya wananchi.
Ningependa
kutoa shukrani za pekee kwa Jamii Forums na watanzania kwa ujumla kwa utambuzi
huu. Majukwaa kama Jamii Forums ni muhimu kwa ajili ya kuleta uwazi na
ushirikiano, na ni matumaini yangu kuwa tutaendelea kushirikiana katika kujenga
jamii bora zaidi.
Kwa upande
wake Mkurugenzi wa Jamii Forums Maxence Melo ameishukuru Serikali na wadau
wengine kwa kuendelea kushirikiana na Jukwaa la Jamii Forums kujibu na kutatua
changamoto mbalimbali za wananchi katika Sekta mbali nchini kwani Jukwaa hilo
limesaidia kuleta suluhu kwa changamoto za wananchi kwa kuoatiwa majibu au
utatuzi na Serikali.
0 Maoni