Rais Samia ahutubia Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Polisi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali kabla ya kufunga Mkutano Mkuu wa mwaka wa Maafisa Wakuu Waandamizi wa Jeshi la Polisi wakati kilele cha maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi hilo, Moshi Mkoani Kilimanjaro tarehe 17 Septemba, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya picha ya kuchora kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Camillus Wambura wakati wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Maafisa Wakuu Waandamizi wa Jeshi la Polisi uliofanyika Shule ya Polisi Tanzania (TPS) Moshi Mkoani Kilimanjaro tarehe 17 Septemba, 2024.

Viongozi Wastaafu wa Jeshi la Polisi la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa kwenye Mkutano Mkuu wa mwaka wa Maafisa Wakuu Waandamizi wa Jeshi la Polisi uliofanyika Shule ya Polisi Tanzania (TPS) Moshi Mkoani Kilimanjaro tarehe 17 Septemba, 2024.

Gwaride la heshima lililoandaliwa na Jeshi la Polisi Tanzania likipita mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi hilo yaliyofanyika katika Shule ya Polisi Tanzania (TPS), Moshi Mkoani Kilimanjaro tarehe 17 Septemba, 2024.

Chapisha Maoni

0 Maoni