NHIF punguzeni matumizi na mdhibiti udanganyifu- Dkt. Mollel

 

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel ameuagiza Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kupunguza matumizi, kutoa elimu,  kuongeza ufanisi na kupambana na vitendo vya udanganyifu ili kuhakikisha wanachama na wananchi  wanapata huduma bora.

Dkt. Mollel ametoa maagizo hayo jana alipokutana na Maofisa Waandamizi wa NHIF, kwenye kikao kazi kilichofanyika Mkoani Arusha kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya uboreshaji wa huduma za matibabu hususan katika kipindi hiki cha kuelekea utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote.

Ametumia fursa hiyo kumpongeza Mkurugenzi Mkuu Dkt. Irene Isaka kwa kuaminiwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuiongoza NHIF hivyo amemhakikishia ushirikiano wa kutosha kutoka kwa viongozi wa Wizara ya Afya ili aweze kutimiza malengo ya utoaji wa huduma bora kwa wanachama na wananchi.



Chapisha Maoni

0 Maoni