Mume akiri kusaidia mkewe kubakwa kwa miaka 50

 

Dominique Pelicot mwanaume wa miaka 71 Mfaransa anayetuhumiwa kumnywesha dawa za usingizi mkewe na kisha kuwaita wanaume wengine wambake kwa miaka 10, amekiri makosa yote yanayomkabili.

Akiwaelezea washirika wenzake 50 wa ukatili huo wa kijinsia kwa aliyekuwa mkewe Gisèle, Pelicot aliiambia Mahakama “Mimi ni mbakaji kama ilivyo kwa wenzangu kwenye hiki chumba”.

Pelicot alieleza kuwa washtakiwa wenzake wanajua kuwa hawana la kusema kinyume chake na kuongeza kuwa mtalaka wake huyo hakustahili walichomfanyia.

Gisèle alipopatiwa fursa ya kuongea, alisema amepata wakati mgumu kusikiliza kauli za aliyekuwa mumewe, "Kwa miaka 50 nimeishi na mwanaume ambaye sikudhani anaweza kunifanyia haya, nilimuamini mno."




Chapisha Maoni

0 Maoni