Mradi wa utafiti wa simba chachu ya utalii Serengeti

 

Taarifa za kisayansi  zinazotokana na Mradi wa muda mrefu wa Utafiti  wa SIMBA SERENGETI unaoratibiwa na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) kupitia  Kituo cha Utafiti wa Wanyamapori Serengeti, zimekua chachu katika uhifadhi  na kivutio   cha Utalii  ndani ya hifadhi  ya  Taifa  Serengeti.

Mradi huu wa SIMBA SERENGETI unafuatilia   idadi, tabia na mienendo ya makundi ya simba kwa zaidi ya miaka 50, ambapo kwa sasa yapo makundi 20 yenye jumla ya simba takribani 300 yanayofuatiliwa.

Aidha, Katika mradi  wa SIMBA  SERENGETI utambulisho hufanyika  kwa kila Simba kuandaliwa kadi maalumu  (Lion  identification  card) kwa kutumia alama/madoa ya Kipekee  kwenye  uso eneo la ndevu (Whisker spots) na  alama nyinginezo za asili.Utambulisho huu husaidia kumfuatilia simba mmoja mmoja ndani ya kundi.

Aidha matumizi ya teknolojia yanarahisisha utafiti wa simba ambapo kwa kutumia mikanda ya simba yenye redio za mawasiliano (VHF/GPS satellite collars) anayofungwa  simba jike katika kila kundi  unasaidia kujua kundi lipo wapi.

Taarifa  za  kisayansi za utafiti  zinatoa dira katika kuwahifadhi  Simba,  kunadi Utalii kupitia takwimu  na  tabia za simba, ikikumbukwa Simba ni Miongoni mwa Wanyamapori wakubwa ambao ni kivutio cha utalii (major tourism attraction) ambaye watalii wengi wanapenda  kumuona wanapokuja kwenye hifadhi.

#Tafiti  za wanyamapori  kwa ustawi wa  uhifadhi na kukuza  utalii  nchini



Chapisha Maoni

0 Maoni