Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),
Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa Tarafa ya Matemanga,
Wilaya ya Tunduru, aliposimama eneo hilo kuwasalimia, majira ya mchana, leo
tarehe 26 Septemba 2024, akitokea Wilaya ya Namtumbo, ambako pia alipata fursa
ya kusimama na kusalimia wananchi maeneo ya Likola, Rwinga na Mchomora.
Mhe. Rais
Dkt. Samia ameingia wilayani Tunduru, akiendelea na ziara yake ya kikazi maeneo
mbalimbali ya wilaya za Mkoa wa Ruvuma, ambayo anaitumia kupata mrejesho wa
wananchi kuhusu mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha
Mapinduzi ya 2020 - 2025, unaofanywa na Serikali ya CCM anayoiongoza, kupitia
huduma na miradi mbalimbali ya maendeleo katika maeneo yao.
Aidha, Mhe.
Rais Dkt. Samia anatumia ziara hiyo kusikiliza changamoto za wananchi na
kuzichukua kwa ajili ya kuzifanyia kazi au kuzitolea maagizo ya ufumbuzi,
kupitia mawaziri na watendaji wa Serikali aliombatana nao ziarani.
0 Maoni