Bodi ya
Makamishna ya Kamisheni ya utalii Zanzibar ikiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi
hiyo Nd. Rahim Bhaloo imetembelea Hifadhi ya Taifa Ruaha Septemba 25,2024.
Dhumuni la
Safari hiyo ni kuangalia fursa mbalimbali zilizopo ndani ya Hifadhi ya Taifa
Ruaha ili kufanya Hifadhi hiyo kuwa moja ya zao la utalii kwa watalii kutoka
nchi mbalimbali wanaotokea Zanzibar.
"Lengo kubwa
linaloambatana na Safari hii ni kuweza kuuza utalii wa Tanzania kwa Vivutio vya
Fukwe na Hifadhi kwa pamoja,"alisema Bhaloo. Na hivyo kuendelea kukuza
ushirikiano baina ya Zanzibar na Tanzania bara.
Kwa upande
wake Mkuu wa Hifadhi, Hifadhi ya Taifa Ruaha, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa
Uhifadhi, Godwell Ole Meing'aki alisema huduma za kitalii katika Hifadhi hiyo
zimekuwa zikiimarika kila siku.
Aliipongeza
bodi hiyo kwa kitendo cha kutembelea Hifadhi ya Taifa Ruaha ambapo alisema
ushirikiano wao na wadau mbalimbali kunachangia shughuli za kitalii katika
hifadhi hiyo kwa ujumla.
Aliongeza
kuwa yapo maeneo mengi ya uwekezaji ndani ya Hifadhi na kuwa Shirika la Hifadhi
za Taifa Tanzania limeweka mazingira rahisi Kwa wawekezaji wa ndani na nje ya
Taifa na kuwa milango ipo wazi Kwa yeyote atakae penda kuwekeza Hifadhi ya
Taifa Ruaha.
0 Maoni