Ugonjwa wa homa ya nyani Mpox umetangazwa kuwa janga la afya la dharura barani Afrika na Kituo Kikuu cha masuala ya Afya Afrika.
Wanasayansi wa Kituo cha Kudhibiti Magonjwa Afrika (CDC) wamesema wameshtushwa na kasi ya kusambaa kwa maambukizi mapya ya ugonjwa huo.
Tangu kuibuka kwa mlipuko wa ugonjwa huo mwaka huu, watu 13,700 wameugua Mpox na 450 wameripotiwa kufa katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Virusi vya ugonjwa huo unaosababisha vipele mwilini, vimesambaa katika mataifa mengine ya Afrika yakiwemo ya Burundi, Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), Kenya na Rwanda.
0 Maoni