Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kufanyika Novemba 27

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Mohamed Mchengerwa ametangaza kuwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa utafanyika Novemba 27, 2024

Akitoa tangazo la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa mwaka 2024 leoa Jijini Dodoma, Waziri Mchengerwa amesema nafasi zinazowaniwa katika uchaguzi huo ni pamoja na Wenyeviti wa Vijiji, Wajumbe wa Halmashauri ya Vijiji, Wenyeviti wa Vitongoji, Wenyeviti wa Mitaa na Wajumbe wa Kamati za Mitaa.

Mhe. Mchengerwa ameeleza kuwa ukomo kwa viongozi waliopo sasa utakuwa ni Oktoba 28, 2024.

Waziri Mchengerwa ameongeza kuwa fomu za wagombea wa nafasi hizo ambao ni kutoka vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu zitaanza kutolewa Novemba Mosi hadi 07, 2024 na kampeni za uchaguzi zitaanza Novemba 20 hadi 26, 2024.

Kufuatia kutangazwa kwa tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi huo wa Serikali za Mitaa, Waziri Mchengerwa  amemuelekeza Mkurugenzi wa TAMISEMI kuhakikisha kuanzia Agosti 16, 2024 elimu ya upigaji kura inaanza kutolewa kwa wananchi ili waweze kufahamu namna ya kushiriki katika uchaguzi huo.

Chapisha Maoni

0 Maoni