Wito huo umetolewa leo jana tarehe 25 Agosti, 2024 na
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe.
Jacobs Mwambegele, wakati akifungua mkutano wa wadau wa uchaguzi uliofanyika
mkoani Mara.
Mhe. Jaji Mwambegele amesema mawakala au viongozi wa vyama
vya siasa hawaruhusiwi kuingilia mchakato wa uboreshaji vituoni kwani kufanya
hivyo ni kwenda kinyume na sheria ya uchaguzi.
Amehimiza viongozi wa vyama vya siasa na wadau wa uchaguzi
kuzingatia sheria ya uchaguzi, kanuni za uboreshaji, maelekezo ya tume, na
kusimamia miiko na mipaka ya uendeshaji wa zoezi la uboreshaji wa Daftari.
Pia amevitaka vyama vya siasa kutumia sheria zilizopo
kuwasilisha changamoto zinazojitokeza kwa tume, ambapo ameongeza kuwa INEC
itazingatia Katiba, sheria ya uchaguzi, na kanuni zilizotungwa chini ya sheria
katika zoezi la uboreshaji.
Akiwasilisha mada kwenye mkutano huo, Mkurugenzi wa Uchaguzi
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Ramadhan Kailima amsema Tume inategemea
vyama vyenye usajili kamili kutumia fursa za kisheria zilizotolewa kwao
kuhakikisha zoezi la uboreshaji linafanikiwa na kuongeza kuwa endapo
kutajitokeza changamoto zozote wakati wa zoezi, Vyama vitumie taratibu
zilizoainishwa kwenye sheria kuwasilisha changamoto hizo.
“Viongozi wa vyama hawapaswi kuingilia utekelezaji wa
majukumu ya watendaji wa vituo wakati wote wa uandikishaji wa wapiga kura
vituoni kama kuomba orodha au idadi ya walioandikishwa au kuboresha au
kuhamisha taarifa zao,”
Ameeleza kuwa, Tume inaowajibu wa kuwapatia vyama vya siasa
taarifa hizo mara baada ya zoezi kukamilika.
Mkutano kama huo umefanyika pia mkoani Simiyu na Manyara
ambapo akifungua mkutano mjini Bariadi, mkoani Simiyu, Makamu Mwenyekiti wa
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, Mbarouk
S. Mbarouk, amewataka wadau kuwaelimisha wananchi kujiandikisha mara moja tu
ili kuepuka uvunjaji wa sheria.
Naye Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa
Mahakama Kuu, Mhe. Asina Omari, ambaye alifungua mkutano wa wadau wa uchaguzi
mkoani Manyara, amewahimiza watu wenye ulemavu, wazee, wagonjwa, wajawazito, na
akina mama wenye watoto wachanga watakaokwenda nao vituoni kujitokeza kwa wingi
kwa kuwa watapewa fursa ya kuhudumiwa bila kupanga foleni.
Mikutano hiyo ni maandalizi ya mzunguko wa nne wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambao utajumuisha mkoa wa Mara, Simiyu na baadhi ya halmashauri za Mkoa wa Manyara ambazo ni Halmashauri ya Mji wa Babati na Halmashauri za Wilaya za Babati, Hanang na Mbulu ambapo uboreshaji utaanza tarehe 04 Septemba, 2024 hadi 10 Septemba, 2024 na vituo vitakuwa vinafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.
0 Maoni