Balozi Polepole afanya mahojiano na Mjane wa Che Guevara

 

Balozi wa Tanzania nchini Cuba Ndugu Humphery Polepole amefanya mahojiano na Mama Aleida March Mjane wa Mwana Mapinduzi Che Guevara.

Kupitia akaunti za mitandao ya kijamii balozi wa Tanzania nchini Cuba ndugu @hpolepole ameposti picha zikionyesha akiwa kwenye mazungumzo na mjane wa Mwana mapinduzi #cheguevara na kuandika.

Nimekuwa na mazungumzo mazuri sana na Mama Aleida March Mjane wa Mwana Mapinduzi Guevara anasema anaikumbuka sana Tanzania 🇹🇿 anasema alikuwa na wakati mzuri sana Tanzania alipokuja kumsalimu Che Nchini Tanzania. Hii habari ya Che Guevara kuwepo Tanzania nitaisimulia wakati mwingine.

Tumezungumza mambo mengi ambayo kadiri muda unavyokwenda nitawajuza lakini mambo mawili kwa hakika 1. Tutakuwa na Mama Aleida March kwenye Kongamano la Kimataifa la Kiswahili - Havana Mwezi Novemba 2024. Ukikosa umekosa vyote! 2.






Chapisha Maoni

0 Maoni