Rais Samia kushiriki Tamasha la Kizimkazi

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kushiriki Tamashaa Kizimkazi 2024 linaloendelea kwenye Uwanja wa Dimbani Mkoa wa Kusini Unguja tamasha ambalo limekuwa na mchango mkubwa katika kuhamasisha Utalii na Maendeleo Visiwani Zanzibar.

Mpaka Sasa Maeneo mengi ya Zanzibar yamefurika Ugeni hivyo kuchochea Shughuli za kibiashara kwanye hotel, migahawa, vyombo vya Usafiri na fursa mbalimbali za kiuchumi.

Tamasha la Kizimkazi lililoasisiwa na Rais Samia katika kuhamasisha utalii na kutangaza utamaduni wa Zanzibar, limekuwa kivutio kikubwa kwa wageni kutoka mataifa ya nje pamoja na kutoka upande wa Tanzania bara.



Chapisha Maoni

0 Maoni