Mutharika aamua kurejea tena kuwania urais mwakani

 

Aliyekuwa Rais wa Malawi Peter Mutharika amechaguliwa kukiongoza chama kikuu cha upinzani cha Democratic Progressive Party (DPP) katika uchaguzi wa rais wa mwakani.

Huku ni kurejea tena kwenye ulingo wa siasa kwa kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 84, ambaye aliiongoza Malawi kwa miaka sita, na baadae kusema kuwa hatawania tena urais.

Mutharika amewashangaza wengi kwa kubadili msimamo wake hivi karibuni, akisema kuwa wafusia wake wanamuhitaji kuiokoa nchi ya Malawi isiharibiwe na Rais Lazarus Chakwera.

Mutharika alishindwa na Rais Chakwera mwaka 2020, katika uchaguzi wa marudio uliotokana na agizo la Mahakama ya Katiba, baada ya kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa mwaka uliopita.

Chapisha Maoni

0 Maoni