Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda amemshukuru Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha
Shilingi Bilioni 7 kuuboresha uwanja wa ndege wa Arusha katika jitihada za
kuufanya uwanja huo kutoa huduma kwa saa 24.
"Mkandarasi ameshapatikana na mkataba umeshasainiwa na
sasa hivi anamalizia usanifu na mkataba ni wa miezi 12 lakini jana
tumekubaliana wamuharakishe kadri inavyowezekana angalau ndani ya miezi nane
awe amemaliza kutufungia taa," alisema Makonda.
Kwasasa uwanja wa ndege wa Arusha unatoa huduma zake mchana pekee, suala ambalo limekuwa kikwazo kwenye jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan za kukuza utalii wa Arusha na Tanzania kwa ujumla hasa wakati huu ambapo kunashuhudiwa wingi wa watalii wanaotokana na filamu ya kuvutia watalii kuja kutalii nchini Tanzania, filamu ya The Royal Tour.
0 Maoni