Mmiliki wa mabasi ya Sauli afariki kwa ajali ya barabarani

 

Mkurugenzi na Mmiliki wa Mabasi ya Sauli Solomon Sauli Mwalabila amefariki dunia Leo 4 August 2024 Kwa ajali gari iliyotokea eneo la Miwaleni, Mlandizi mkoani Pwani.

Kamanda wa Polsi Mkoa wa Pwani Pius Lutumo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza kuwa ilihusisha magari matatu, (malori mawili na gari dogo moja).

Amesema ajali hiyo ilisababishwa na lori aina ya Fuso lililofeli breki na kuligonga gari dogo aina ya Jeep ambalo nalo liligonga lori  jingine aina ya Vowo lililokuwa limebeba kokoto.

Chapisha Maoni

0 Maoni