Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa upanuzi wa Kiwanda cha Sukari Kilombero (K4), tarehe 4 Agosti, 2024.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kiwanda cha Sukari Kilombero wakimtazama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) wakati alipoweka jiwe la msingi la upanuzi wa Kiwanda cha Sukari Kilombero.
Muonekano wa ujenzi wa upanuzi wa Kiwanda cha Sukari Kilombero uliozinduliwa leo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka jiwe la msingi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga wakati alipotembelea Kituo cha Kupoza Umeme Ifakara ikiwa sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro, tarehe 4 Agosti, 2024.
Muonekano wa Kituo cha Kupoza Umeme Ifakara kilichotembelewa leo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ikiwa sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro, tarehe 4 Agosti, 2024.
0 Maoni