Tanki la mafuta na gesi limelipuka Kata ya Kisukuru wilayani Ilala, wakati mafundi wakichomea na kuleta maafa kwa fundi mmoja aliyetambulika kwa jina la Hassan Salehe na fundi mwingine hali yake mbaya.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Kanda
Maalum Dar es Salaam Jumnne Mulilo, amethibitisha tukio hilo ambapo amesema
alipata taafa ya mlipuko wa tanki hilo la mafuta ambalo limeleta kizaa zaa kwa
nyumba zaidi ya 11 kuvunjika vyoo, milango na Singibord mara baada tanki la mafuta kulipuka katika
sehemu ya kuifadhi magari ambayo imejengwa katika makazi ya wananchi.
"Ni kweli jana majira ya saa moja jioni nilipokea
taarifa ya mlipuko wa gesi uliolipua tanki la mafuta Kisukuru Wilaya ya Ilala
na kusababisha kifo cha Fundi Hassan Salehe, aliyekuwa akichomelea na kijana
mwingine hali yake mbaya bado yupo hospitali wote walipata madhara katika
mlipuko wa tanki la mafuta," Kamanda Mulilo.
Kamanda Jumanne Mulilo, alisema madhara mengine yaliotokea
katika mlipuko huo wa tanki la mafuta na mtungi wa gesi nyumba zaidi ya 11
zimevunjika vyoo na milango kutokana na mtikisiko wake kuwa mkubwa.
Kamanda Mulilo alisema Mmiliki wa sehemu hiyo ya kuifadhi
magari anaitwa Juma Jabir, Kabila lake Msambaa na Jeshi la Polisi linaendelea
na uchunguzi wake kwa sasa.
Diwani wa Kata ya Kisukuru Lucy Lugome ,alisema janga hilo la mlipuko ulitokea jana ambapo
umesababisha kifo cha mtu mmoja na nyumba 14 kupata madhara ambapo kwa sasa
Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Ilala imeunda
tume maalum kwa ajili ya kuchunguza tukio hilo.
Diwani Lucy Lugome aliwataka wakazi wa Kisukuru Magoza kuwa
wavumilivu katika janga la ajali hiyo wakisubiri Serikali kumaliza kufanya
uchunguzi wake.
Waziri Mstaafu wa Serikali ya awamu ya nne Hamza Abdalah
Mwinyigoha, ambaye anaishi eneo la tukio hilo alisema wakati mlipuko unatokea
nyumbani kwake wajukuu walikuwa hawapo endapo wangekuwepo maafa yangekuwa
makubwa kwani Mara baada mlipuko huo nyumba yake imepata madhara makubwa
milango kupasuka na vyoo kuvunjika kwa madirisha.
Hamza Abdalah Mwinyigoha alisema katika nyumba yake athari
kubwa imetokea ikiwemo kuharibu Mali na vitu vya thamani.
Alisema ameshangazwa gereji hiyo kubwa kukaa katika makazi
ya wananchi hivyo wameomba Serikali iweze kuchukua hatua kwa ajili ya usalama
wa wananchi wa eneo hilo la Kisukuru.
Mjumbe wa Shina namba 8 Kisukuru Magoza Frola Mwakanyamale, alisema tukio limetokea jana Agosti 27 nyumba yake inapakana na sehemu ya tukio ambapo anamshukuru Diwani wake Lucy Lugome kwa kuwakimbilia na kutoa msaada wa Haraka.
Na Heri Shaaban- ILALA
0 Maoni