MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Mbunge wa Ruangwa, Kassim Majaliwa ameshuhudia wanachama 24 wa vyama vya CUF na ACT-Wazalendo wakirejea CCM ndani ya siku mbili.
Mheshimiwa Majaliwa alishuhudia wanachama hao wakikabidhi
kadi zao kwa Katibu wa CCM wa Wilaya ya Ruangwa, Bw. Abbas Mkwenda (Agosti 23
na 24, 2024) wakati akizungumza na wakazi wa vijiji vya Mtondo (Kata ya
Nambilanje) na Namikulo (Kata ya Chunyu), wilayani Ruangwa, Lindi ambako
alifanya ziara ya jimboni kwake.
Katika kijiji cha Mtondo, wanachama tisa wa CUF walirejesha
kadi zao wakiongozwa na Mzee Bakari Abdallah Nanyambo ambaye alikuwa Mwenyekiti
wa CUF Kata ya Nambilanje. Wengine ni Abdallah Ally Manjawila, Bakari Ally
Nyanga, Bakari Abdallah Nampota, Mwanahawa Abdallah Komaje, Zaituni Omary
Mitachi, Mwanahawa Rashid Chomwingo, Somoe Omary Mkupete na Amina Musa Pachela.
Katika kijiji cha Namikulo, wanachama watano wa
ACT-Wazalendo walikabidhi kadi zao wakiongozwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa ACT
Kata ya Chunyu, Bw. Rashid Ibrahim Nakotyo. Wengine kutoka chama hicho ni
Jafari Ali Namkwacha, Maulid Juma Mbanda, Mwajibu Saidi Baluya na Sefu Salum
Makukuta.
Wengine 10 waliohama kutoka CUF ni Juma Abdalla Ching’oma
(Mwenyekiti wa Kata), Said A. Mnunguye, Mohamed Selemani Lipei, Zena Rajabu
Kabanda, Mohamed Mhumbila, Ally Mohamed Maluva, Abdalla M. Mbandula, Mwanaidi
Saidi Mpingo, Idi Abdalla Matwani na Said Juma Mkomole.
Akizungumza baada ya kupokewa, Mzee Bakari Abdallah Nanyambo alisema ana uzoefu wa miaka 31 kwenye mageuzi na kwa sehemu kubwa alikuwa meneja wa kampeni kwa hiyo yuko tayari kutumia uzoefu wake akiwa ndani ya CCM.
0 Maoni