Mloganzila kufanya kambi ya upandikizaji nyonga na magoti Agosti 26-30, 2024

 

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila itafanya kambi maalum ya ubingwa bobezi ya upasuaji wa upandikizaji nyonga na magoti kwa muda wa siku tano kuanzia tarehe 26 hadi 30 Agosti, 2024.

Kambi hiyo itafanyika kwa kushirikiana na jopo la madaktari wabobezi katika eneo la upandikizaji wa nyonga na magoti wa Muhimbili Mloganzila kwa kushirikiana na Dkt. Venuthuria Ram Mohan Reddy kutoka nchini India ambaye ana uzoefu katika eneo la nyonga na magoti kwa zaidi ya miaka 30.

Kwa wale watakaotaka kupata maelezo zaidi ya kambi hii wanaweza kuwasiliana na Dkt. Joseph Amos 0683680522, Dkt. Shilekirwa Makira 0765958302 au Dkt. Abubakar Hamis 0715219175.

Chapisha Maoni

0 Maoni