Mafuru asisitiza Watanzania kutembelea vivutio vya utalii

 

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bw Ephraim Mafuru, amesisitiza Watanzania waendelee kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii vilivyopo nchini pia kuangalia fursa za Uwekezaji haswa katika nyanja ya Utalii.

Bw. Mafuru ametoa kauli hiyo baada ya kutembelea Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii katika Maonesho ya Wakulima maarufu kama Nanenane yanayofanyika katika Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.

Bw. Mafuru amechukua nafasi hii kuendelea kupongeza juhudi za Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuifungua Tanzania ambapo Wiki iliyopita alizindua Rasmi Reli ya Kisasa ya Kimkakati (SGR) itakayorahisisha Usafiri kati ya Mikoa ya Pwani na Kanda ya Kati. Reli hii itakua chachu ya Maendeleo ya Kilimo, Viwanda, Utalii na Biashara.

Aidha, Bw. Mafuru ametoa wito kwa wadau wote wa Utalii kushiriki katika Onesho la 8 la SITE Mnamo Oktoba 2024.



Chapisha Maoni

0 Maoni