Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde amesema Wizara ya
Madini imekubaliana na Ofisi ya Rais TAMISEMI kukutana na kutatua changamoto ya
tozo zinazowekwa na Halmashauri kwa wachimbaji wa madini nchini.
Mavunde ameyasema hayo mkoani Morogoro katika kikao chake
wachimbaji wa Mkoa wa Morogoro kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero zao
Akizungumza Mavunde amesema “niamesikiliza kwa umakini
mkubwa kilio hicho cha tozo za Halmashauri na tozo nyinginezo kwa wachimbaji
wadogo, kero hizo sio tu kwa wachimbaji wa Morogoro zipo maeneo yote nchini”.
"Tunayo maelekezo ya Mh Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Majaliwa kwamba Wizara hizi mbili zikutane kushughulikia suala hili,"
amesema na kuongeza
"Nataka niwahakikishe mimi na Mwenzangu Mh. Mohamed
Mchengerwa tumekubaliana mara baada ya
ziara ya Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan mkoani Morogoro tutaitisha kikao cha
pamoja ili kushughulikia suala hilo," amesema Mavunde.
Aidha, amewahakikishia wachimbaji wa Morogoro juu ya dhamira
ya Mh. Rais Samia kuongeza nguvu kwenye eneo la Utafiti wa Madini ambapo na
mkoa wa Morogoro pia utanufaika.
Mh. Mavunde ameipongeza Ofisi ya Madini Mkoa wa Morogoro kwa
kuvuka lengo la ukusanyaji maduhuli kufikia Sh Bilioni 4.9 zaidi ya lengo
lililowekwa la Sh bilioni 4.2.
Awali, akisoma risala kwa niaba ya wachimbaji, Mwenyekiti wa Chama cha Wachimba Madini Mkoa wa Morogoro. (MOREMA) Dkt. Omar Mzeru ameshukuru Rais Samia kwa kutoa mashine za uchorongaji kwa wachimbaji wadogo na kutumia fursa hiyo kumuomba Waziri wa Madini kushughulikia changamoto kubwa inayotokana na uwepo wa tozo nyingi zinatozwa na Halmashauri na Taasisi nyingine za serikali kwakuwa zimekuwa zikiwarudisha nyuma kimapato wachimbaji wadogo.
0 Maoni