Kaya zingine 79 na mifugo yao zahama kwa hiari Ngorongoro

 

Kundi jingine la wananchi wanaoishi katika eneo la hifadhi ya Ngorongoro limeondoka leo katika hifadhi hiyo na kuhamia kwa hiari Msomera, mkoani na Tanga na maeneo mengine nchini Tanzania waliyoyachagua kuishi.

Kundi hilo ni mwendelezo wa wananchi wanaoishi eneo la hifadhi ya Ngorongoro kupatiwa elimu na kuamua kwa hiari yao kuondoka kwenye hifadhi hiyo bila ya kushurutishwa baada ya kuelewa nia njema ya Serikali katika kuihifadhi hifadhi hiyo ya Ngorongoro kwa manufaa ya taifa.

Zoezi hilo la kuhama kwa hiari limefanyika leo katika ofisi za zamani za Mamlaka ya Hifadhi ya Ngongoro (NCAA), Karatu mkoani Arusha na limehusisha Kaya 79 zenye watu 367 na mifugo yao takriban 995.



Chapisha Maoni

0 Maoni