Wapanda mlima Wasauzi wafika kilele cha Kilimanjaro

 

Rais wa Afrika Kusini Cyril Pamaphosa amelipongeza kundi la wapanda mlima kutoka Afrika Kusini kwa kufanikiwa kufika kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro.

Katika ujumbe wake kupitia akaunti yake ya  X, Rais Ramaphosa amesema kundi hilo limefanikiwa kufika kwenye kilele cha mlima huo mrefu zaidi barani Afrika.

Kundi hilo la wapanda milima kutoka Afrika Kusini, limefanya hivyo kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa Baba wa Taifa hilo Nelson Mandela Julai 18, 1918 pamoja na miaka 30 ya Uhuru.

Chapisha Maoni

0 Maoni