Wataalam wa shirika la UNESCO waliowasili Tanzania kuhalalisha tena Jiopaki ya Dunia ya UNESCO Ngorongoro-Lengai, wametembelea tarafa za Karatu na Eyasi na kukutana na jamii ya Wairaqw, Wahadzabe na Wadatoga katika kuangalia utekelezaji vigezo vya UNESCO katika kulinda tamaduni za kipekee, jiolojia na ikolojia ya urithi wa eneo hilo.
Katika ziara yao hiyo iliyoanza jumatatu ujumbe huo
ulitembelea eneo la Makumbusho ya UNESCO Jiopaki ya Ngorongoro-Lengai na
kutembelea shule ya awali na ya msingi ya lugha ya Kingereza ya Tumaini na kisha
shule ya awali na ya msingi ya lugha ya Kingereza Father Lieberman zote
zilizopo Karatu kuangalia jitihada za utoaji elimu zenye kuwajengea msingi
vijana kuwa walinzi wa jiopaki.
0 Maoni