Trump arejea nyumbani baada ya kutibiwa jeraha la risasi

 

Mgombea urais wa Marekani Donald Trump amerejea nyumbani kwake New Jersey baada ya kujeruhiwa katika jaribio la kumuua akiwa kwenye mkutano wa hadhara hapo jana.

Milio ya risasi ilisikika wakati akihutubia kwenye hafla iliyofanyika Pennsylvania, na kuibua taharuki kwa umati wa watu, huku askari wa ulinzi wakimzingira na kumtoa jukwaani rais huyo wa zamani.

Trump, ambaye alionekana kuchuruzika damu usoni, amesema amepigwa risasi sikio la kulia na kueleza alizikia mvumo wa kitu na kisha risasi ikatoboa ngozi ya sikio.

Shirika la Ujasusi la Marekani FBI limesema limemtambua aliyefanya shambulizi hilo la kutaka kumuua Trump, kuwa ni Thomas Matthew Crooks (20).

Walinzi waliokuwa katika mkutano huo walimua kwa kumpiga risasi kijana huyo mara tu baada ya kumbaini. Watu wengine wawili waliokuwa kwenye mkutano huo wameripotiwa kujeruhiwa.

Chapisha Maoni

0 Maoni