Taasisi ya Mkapa itaendelea kuunga mkono juhudi za serikali- Dkt. Mwinyi

 

Msarifu wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Taasisi ya Benjamin William Mkapa itaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kuchangia kuandaa nguvu kazi, kuwaendeleza na kuboresha mifumo kupitia programu ya Mkapa Fellows katika sekta ya afya.

Dkt. Mwinyi aliyasema hayo leo tarehe 31 Julai 2024 wakati wa kumbukizi ya tatu ya Hayati Benjamin William Mkapa katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.

Aidha Rais Dkt. Mwinyi ameleeza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatarajia kujenga Hospitali ya Rufaa ya Binguni itakayokuwa na vitanda 600 hivi karibuni.

Halikadhalika Rais Dkt. Mwinyi amesema SMZ imetoa ajira mpya 1,050 za watumishi wa afya, imejenga  jumla ya nyumba 80, 16 kila wilaya zilizogharimu shilingi bilioni 20  ili kuboresha mazingira ya kazi kwa watumishi wa sekta ya afya na kuwapa motisha ya kazi.

Vilevile Rais Dkt. Mwinyi amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan  kwa juhudi anazochukua za kuboresha sekta ya afya nchini.





Chapisha Maoni

0 Maoni