Miss Travel World Czech Republic awasili nchini

 

Miss Travel World Czech Republic 2024,  Julie Hojdyzovà awasili Tanzania jana katika uwanja wa ndege wa Kilimanjaro KIA, na kupokelewa na mwenyeji wake Sam Malugu, Rais wa Miss Travel World Tanzania.

Miss Julie anategemea kuungana na warembo wengine kutoka mataifa saba kwa ajili ya uzinduzi wa shindano la kimataifa la Miss Travel World 2024 itakayofanyika tarehe 9 August 2024 katika hoteli ya Parrot Arusha.

Lengo la shindano hilo ni kuunga mkono jitihada za Rais wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan katika kutangaza utalii kikataifa kama alivyofanya kupitia filamu ya THE ROYAL TOUR.  Wakiwa nchini warembo hao watatembelea vivutio mbalimbali vya utalii.

Chapisha Maoni

0 Maoni