Rais Samia amteua na kumuapisha Mkurugenzi Mkuu mpya wa TISS

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Bw. Suleiman Abubakar Mombo kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Julai, 2024.

TRAARIFA:

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemteua na kumuapisha Bw. Suleiman Abubakar Mombo kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Taarifa fupi iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikuku Sharifa Nyanga imesema Momba anachukua nafasi ya Balozi Ali Idi Siwa ambaye amestaafu.

Kabla ya uteuzi huo Bw. Suleiman Abubakar Mombo alikuwa Afisa Mwandamizi wa Ofisi ya Rais, Ikuku.

Chapisha Maoni

0 Maoni