Rais Ruto avunja baraza lake la mawaziri

 

Rais William Ruto wa Kenya amevunja baraza la mawaziri pamoja na kumuengua Mwanasheria Mkuu Justin Muturi, kufuatia shinikizo la maandamano ya vijana kuipinga serikali.

Katika uamuzi wake huo alioutangaza hivi punde, ni waziri mkuu aliyesalimika, Musalia Mudavadi, ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya.

Rais Ruto amesema atawahusisha wadau wengine wa vyama vya siasa katika mchakato wa kuunda baraza la mawaziri.

Pamoja na mambo mengine Rais Ruto amesema kuanzia wizara zote zitakuwa chini ya Katibu Mkuu Kiongozi.


Rais wa Kenya William Ruto akiwa kwenye picha ya pamoja na baraza lake la mawaziri ambalo amelivunja rasmi hii leo tarehe 11/07/2024.



Chapisha Maoni

0 Maoni