Rais Mstaafu Kikwete ajionea wanyama mbalimbali Sabasaba

 

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ametembelea eneo maalum lenye wanyama hai (Animal Kingdom) katika Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii lilipo kwenye Viwanja vya Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea Dar es Salaam.

Dkt. Kikwete aliyepokewa eneo hilo jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, alionesha kufurahia wanyama mbalimbali waliopo eneo hilo kuanzia Simba, chui, swala, nyumbu, pofu, mamba, fisi, kenge na ndege aina mbalimbali.

Mamia ya wananchi wanaotembelea Sabasaba pia hupita katika banda hilo kujionea wanyama asilia kutoka hifadhi na mapori mbalimbali ya akiba hapa nchini huku wengi wakisema wanatembelea maeneo hayo kama utalii wa ndani kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyefanya hivyo kwa kushiriki filamu ya “Tanzania: The Royal Tour.”



Chapisha Maoni

0 Maoni