Paul Kagame ashinda kwa kishindo uchaguzi wa rais

 

Rais Paul Kagame wa Rwanda ameshinda uchaguzi wa urais kwa ushindi wa kishindo baada ya kura karibia zote kukamilika kuhesabiwa katika uchaguzi uliofanyika jana.

Hadi sasa anaongoza kwa asilimia 99.15 ya kura, zikiwa zimehesabiwa asilimia 79 ya kura, katika matokeo ya awali yaliyotolewa na tume ya uchaguzi.

Kiongozi huyo wa Rwanda mwenye umri wa miaka 66, hakuwa akikabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa wagombea wengine wawili wa urais.

Kagame ambaye amakuwa madarakani kwa miaka 24, amewashukuru wananchi wa Rwanda wakati akiongea akiwa Makao Makuu ya Chama cha Rwandan Patriotic Front (RPF).

Chapisha Maoni

0 Maoni