Mkurugenzi wa Walinzi wa Rais ajiuzulu kwa kupigwa risasi Trump

 

Mkurugenzi wa walinzi maalum wa rais na marais wastaafu Secret Service, Bi. Kim Cheatle amejiuzulu wadhifa wake kufuatia jaribio la kumuua aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump.

Bi. Cheatle alitoa maelezo yake kwa muda wa karibu saa sita mbele ya kamati ya bunge ya masuala mahususi jumatatu.

Wabunge walionekana kukerwa mno kwa kukataa kujibu swali kuhusu kupigwa risasi Trump kwenye kampeni huko Butler, Pennsylvania mapema mwezi huu.

Katika barua yake ya kujiuzulu Bi. Cheatle ameandika, “Kama Mkurugenzi wenu, Nakubali kuwajibika kwa kushindwa kutimiza majukumu ya ulinzi.”

Chapisha Maoni

0 Maoni