Dkt. Tulia na Rais Putin wazungumzia kuimarisha amani

 

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Urusi, Vladimir Putin leo Jijini St. Petersburg nchini Urusi ambapo wamejadili kuhusu namna bora ya kuimarisha amani duniani.

Akizungumzia kuhusu mgogoro unaoendelea baina ya Urusi na Ukraine, Dkt. Tulia amesema kabla ya kuzungumza na Rais Putin, tayari walishazungumza na maspika wa nchi hizo mbili, ambapo wao kama IPU wamezungumza naye kama kiongozi wa nchi katika sura ya kuiziweka nchi hizo mbili pamoja.

Pamoja na mambo mengine, Dkt. Tulia amesema wao kama Umoja wa Mabunge Duniani, wanatarajia kutengeneza fursa ya mabunge ya Urusi na Ukraine kuweza kuzungumzia amani katika maeneo yao ya utawala.



Chapisha Maoni

0 Maoni