Operesheni ya Madada Poa haipoi Dar- Chalamila

 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ameendelea kusisitiza suala la operesheni ya kuwakamata wanawake wanaojiuza (Madada poa) lililoanzishwa na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hassan Bomboko kwa kuseama ni zoezi endelevu na litaendelea kufanywa na wakuu wote wa Wilaya za Dar es Salaam ili kukomesha vitendo vya uvunjifu wa maadili mitaani.

“Suala la operesheni za madada poa huo ni mwanzo tu litaendelea sana, tumeshapokea malalamiko kutoka kwa wazazi kwamba watoto wao wanapokwenda shuleni wanashuhudia vitu ambavyo ni kinyume na maadili,” alisema Chalamila akiongea na waandishi wa habari hii leo.

Ndugu yetu Bomboko kamwe hayuko peke yake, mimi ndiye Kaka yake mkubwa wa mkoa huu niko hatua tano mbele, yuko hatua chache nyuma, yuko kulia kwangu yuko kushoto kwangu na Wakuu wa wilaya wote wa mkoa wa Dar es Salaam wataendelea kufanya shughuli hizo, alisema.

Chapisha Maoni

0 Maoni