Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Emmanuel
Nchimbi, ameelezea umuhimu wa ushirikiano unaovinufaisha vyama vya CCM na Chama
cha Kikomonisti cha China (CPC) katika kikao chake na Mjumbe wa CPC Komredi
Tang Degjie kilichofanyika Makao Makuu ya CCM Dar es Salaam.
Dk. Nchimbi ameelezea kuwa urafiki wa muda mrefu uliopo
baina ya Tanzania na China, ulioimarika chini ya uongozi wa vyama vya CCM na
CPC, umeendelea kudumu kwa zaidi ya miongo sita ya uhusiano wa kidiplomasia.
"Ushirikiano wa vyama vyetu hivi viwili ulianzishwa na
waasisi wa mataifa yetu, Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Mwenyekiti Mao Zedong,
na tangu hapo umekuwa na kujikita katika ushirikiano wa kimkakati,” alisema
Dkt. Nchimbi.
Dk. Nchimbi ameangazia mafanikio ya ushirikiano huo katika sekta ya ujenzi, afya, utalii, kilimo, madawa, biashara na uchumi, na kuhimiza China kuiunga mkono Tanzania kwa kuwekeza katika sekta zinazoanza kukua.
0 Maoni